Dully Sykes hana mpango wa kuoa

0
13

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa kwasasa hana mpango wa kufunga ndoa licha ya kubezwa kwa kutofunga ndoa.

Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa suala la kuoa ni jambo dogo na watu wasipende kulichukulia kwa ukubwa huo mpaka kumuandama kwa kutokufunga ndoa.

Amesema kuwa unajua kuhusu suala la nitaoa lini huwa naulizwa sana eti nichukue mke kwa sababu nazeeka, naomba leo niwaambie watu kwamba suala la kuoa ni kitu kidogo sana wala wasipende kulichukulia kwa ukubwa kiasi hicho.

Pia amesema kuwa “Unajua hata kwa Mungu siyo ibada ya kusema kwamba eti mimi nitahukumiwa eti kwa sababu sijaoa, sitaki kuulizwa tena swali hili,”.

Mwanamuziki huyo hajawahi kufunga ndoa licha ya kuwa na watoto aliozaa na wanawake tofauti tofauti.

LEAVE A REPLY