Dully Sykes aweka wazi Harmonize kutumia mistari yake

0
58

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes maarufu kama Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa amefurahi baada ya Harmonize kutumia baadhi ya mistari ya wimbo wake.

Dully ameamua kufafanua hilo baada ya mashabiki kuanza kurusha maneno kwa Harmonize kuwa ameiba mistari ya Dully kwenye wimbo wake huo mpya.

Harmonize ametumia melody ya wimbo Dully Sykes wa muda mrefu unaofahamika kama ‘Handsome’ katika wimbo wake mpya alioutoa wa Kainama na kusema amefurahi kwa sababu ameona kama amemuenzi.

Dully amesema kabla Harmonize hajaweka maneno katika wimbo huo, alimshirikisha kwanza na hata wakati anarekodi alikuwepo studio na akamshauri baadhi ya vitu hivyo yeye amefurahi kuona mashairi yake yanaimbwa na mwanamuziki mwingine.

Harmonize ametumia mistari ya wimbo huo kwenye wimbo wake mpya aliowashirikisha wasanii wenzake Diamond Platnumz na Burna Boy kutoka nchini Nigeria.

Msanii huyo amesema kuwa hajachukulia kama amemuibia mistari yake kwasababu amemuambia mwenyewe atumie mistari hiyo kwenye wimbo wake huo mpya.

LEAVE A REPLY