Dully Sykes: Alikiba hakunialika kwenye harusi yake

0
350

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa hajaalikuwa kwenye harusi ya msanii mwenzake Alikiba ambaye kwa asilimia kubwa amehusika kwenye sanaa yake ya muziki mpaka kufikia alipo sasa.

Dully Sykes amesema hajapewa taarifa yoyote kutoka kwa Ali Kiba licha ya kuwa mtu wake wa karibu, zaidi ya kuona mitandaoni na kuthibitishiwa na watu wa Mombasa.

Hata hivyo Dully Sykes amesema anamtakia Alikiba maisha mema kwenye ndoa yake, kwani ni jambo la heri na kumsihi asichukulie mzaha suala la ndoa.

Amesema kuwa “Namtakia ndoa njema, nampenda sana na anajua, namtakia maisha mema, na namsihi ndoa sio kitu kidogo, anapoamua kuchukua mtoto wa watu, hasa ambaye amemchukua nchi nyingine, inabidi amuheshimu sana, amuonyeshe upendo hata yule mtoto akiitwa na wazazi wake mbona huji kutuangalia akose cha kuwaambia kwa upendo atakaompa”,.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Alikiba anatarajia kuoa hivi karibuni, ndoa ambayo imetangazwa kufanyika kwa siri nchini Kenya mjini Mombasa, na mpaka sasa mwanamke anayetarajia kuolewa na Alikiba hajajulikana ni nani kwa picha.

LEAVE A REPLY