Dully Sykes afunguka sababu ya kufungua studio

0
331

Mwanamuziki wa mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema kuwa ameamua kufungua studio yake mwenyewe ili kuepuka usumbufu wa kurekodi nyimbo zake.

Dully amefunguka hayo hivi karibuni na kudai kuwa wasanii wanapata pesa lakini wengi wao wanaendekeza starehe sana na kusahau uwekezaji kitu ambacho yeye aliepukana nacho kwa kuhofia kupata kero kwenye shughuli zake binafsi.

Dully amesema kuwa “Nilifikiria nikaona kwamba nafanya muziki, kama napata idea siwezi kwenda kumgongea mtu nikamwambia kwamba naomba kurecord wakati mtu kajipumzika No! kama nina studio yangu naweza kurecord mwenyewe”.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Sisi wasanii tunapata hela, wasanii wanapenda starehe tu. Kwahiyo Equipments ni vitu ambavyo unaweza kununua kama ukiwa na akili hata kwa hela ndogo unayoipata” .

Dully ameongeza kuwa baada ya kupiga hatua mpaka kumiliki bendi na vifaa vya studio vyenye viwango ameona ni vyema kuanzisha record lebo hatua ambayo ameitaja kama moja mafanikio ya muziki wake kwa kipindi chote cha kufanya muziki.

LEAVE A REPLY