Dully Sykes afunguka changamoto za mahusiano yake

0
120

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa alichanganyikiwa baada ya kuachwa na mpenzi wake ambaye ni mama mtoto wake.

Dully Sykes amesema aliathirika baada ya kuachwa hali iliyompelekea kulala chini hadi leo hii na vitu vyote walivyonunua na mwanamke huyo, amevigawa kwa watu ili mradi asiendelee kumkumbuka.

Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa “Mama wa mtoto wangu wa tatu aliniacha, kwa sababu tulikuwa tunaishi wote kwa muda mrefu bila kufunga ndoa, alivyoondoka sikuamini na iliniathiri hadi nilichanganyikiwa.

Pia Dully amesema kuwa meza ya vipodozi aliyokuwa anatumia nikaigawa, kitanda ambacho tulikuwa tunakilalia nikakigawa pia hadi leo nalala chini”.

Mwanamuziki ni moja ya wasanii wakongwe hapa nchini ambao wameutoa mbali huu muziki wa Bongo Fleva toka miaka ya 2000 hadi sasa anaendelea kutamba.

LEAVE A REPLY