Dullah Makabila aamua kuyakimbia mapenzi

0
266

Mwanamziki wa Singeli Dullah Makabila amesema mwaka huu hataki kuendekeza suala la wanawake ingawa anaamini kuwa kama ni warembo wapo tu na ataapata.

Makabila ambaye alikuwa akijihusisha kwenye mapenzi na muigizaji Husna Sajent, amesema kwamba kwav sasa yupo single na kwamba ameelekeza nguvu zake kwenye m,uziki wake kwani mwaka uliopita alishindwa kufanya kazi nzuri kutokana na kuandamwa na skendo.

Pamoja na hayo Makabila amesema mbele ya kamera za eNEWZ kwamba licha ya wasichana wengi kumtaka kimapenzi kutokana na muonekano wake hataki tena mapenzi yachukue nafasi maishani mwake

Mbali na hayo Msanii huyo amesema sababu kubwa ya yeye kuchelewa kutoa nyimbo mpya ni kutokana na kazi nyingi alizokuwa anazipata hapo nyuma hali iliyomfanya kutengeneza mkwanja mrefu mpaka kupoteza mawazo mapya ya kutengeneza nyimbo mpya zenye mvuto.

LEAVE A REPLY