Dudubaya: Kuacha matumizi ya madawa ya kulevya ni dhamira ya mtumiaji tu na si vingine

0
93

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amesema ili mtu aweze kuacha madawa ya kulevya ni hadi dhamira yake imsute na kuamua mwenyewe kwa dhati na si kushawishiwa na mtu.

Dudubaya amesema msanii mwenzake Chid Benz na wasanii wengine hawawezi kuacha kutumia madawa ya kulevya kwa watu kuwapeleka popote kama dhamira yao haijawasuta kuhusu jambo hilo.

Dudubaya amesema “Kama una mtoto ambaye ni changudoa hata ufanye nini kama dhamira yake haijamsuta akaamua kwa dhati kutoka moyoni mwake hataacha atakuwa anaruka hadi ukuta ndivyo ilivyo kwa watu ambao wameshajiingiza kwenye madawa ya kulevya”.

Kauli hiyo ya Dudubaya inakuja kufuatia baadhi ya wanamuziki wa Bongo fleva kujihusisha katika vitendo vya matumizi ya madawa ya kulevya mpaka kupelekea kupelekwa rehab.

LEAVE A REPLY