Dudubaya afutiwa usajili na Basata

0
118

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kusitisha usajili wa Msanii, Godfrey Tumaini (Dudubaya) leo Aprili 16 kutokana na utovu wa nidhamu.

Hatua imetokana na kitendo cha msanii huyo kutumia lugha za matusi kwa wadau wa sanaa kupitia akaunti yake ya Instagram huku akitambua fika kuwa yeye ni msanii aliyesajiliwa na BASATA.

Kupitia barua iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza amesema kuwa baraza limechukua hatua hizo baada ya msanii huyo kutoa maneno machafu kwa wadau wa Sanaa katika mitandao ya kijamii.

“Dudu Baya amekuwa anatoa kauli zisizofaa kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni, hivyo BASATA linasisitiza kuwa msanii anaposajiliwa hutakiwa kuwa raia mwema na mfano wa kuigwa na jamii kwani msanii ni kioo cha jamii”, amesema Mngereza.

Mngereza ameongeza kuwa wasanii wote wanatakiwa kutokiuka taratibu na sheria zilizopo ili kujiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Baraza hilo.

LEAVE A REPLY