Dudu Baya ashikiliwa na Jeshi la Polisi kisa Ruge

0
227

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dudu Baya anashikiliwa na jeshi la polisi Oyster Bay kwa amri ya waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, huyo amefika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alilielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua ‘Dudu Baya’ kwa kumdhihaki Ruge ambaye alifariki Afrika Kusini.

Dudu Baya alimjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.

Dudu Baya amekuwa akitoa maneno yasikuwa ya kingwana kwa marehemu Ruge kinyumbe na tamaduni za Tanzania kwa marehemu.

LEAVE A REPLY