Drake kuwarudishia fans viingilio baada ya Travis Scott kudondoka jukwaani

0
190
Drake

Staa wa Canada Drake, ameahidi kuwalipa mashabiki 20,000 waliojitokea kutazama shoo yake na Travis Scott kwenye jiji la London baada ya Scott kudondoka jukwaani na kushindwa kuendelea na onyesho.

Scott mwenye miaka 24 alikuwa msanii mualikwa kwenye onyesho hilo na alitakiwa kuungana na Drake kwenye performance ya London ambayo ni sehemu ya ziara yake anayoiita ‘Boy Meets World’.

Scott alidondoka wakati wakiimba wimbo wa Goosebumps wakati alipojikwaa kwenye kishimo kilichopo katikati ya jukwaa ambacho kimeharibu sehemu hiyo ya jukwaa.

Baada ya kuanguka aliondoka jukwaani kwa muda kabla ya Drake kumrudisha tena.

Hata hivyo alishindwa kuendelea na shoo hiyo ingawa hakuonekana kuumia sana.

Baada ya tukio hilo, Drake aliwatangazia mashabiki wake, ‘Ni bure usiku wa leo’, ‘mtalipia siku nyingine’.

Na mwishoni mwa onyesho alisikika akiwaambia mashabiki. “London England, I love you, I hope you enjoyed your free show”.

Hata hivyo bado menejiment yake haijatoa kauli yoyote kuhusiana na maneno hayo ya Drake na hivyo haijajulikana endapo mashabiki hao waliokusanyika kwenye uwanja wa O2 watarudishiwa pesa zao za kiingilio.

LEAVE A REPLY