Drake ashinda tuzo 12 za Billboard

0
330

Mwanamuziki wa Marekani, Drake amekuwa msanii wa kwanza kuwa na tuzo 27 za Billboard baada ya usiku wa kuamkia leo kushinda tuzo 12 katika vipengele tofauti.

Baada ya kushinda tuzo hiz Drake kwasasa ndiyo msanii mwenye tuzo nyingi za Billboard ambazo mpaka sasa anatuzo 27, na kuweza kufanikiwa kumpiku mwanadada Taylor Swift, ambaye yeye alikuwa akishikilia nafasi hiyo kwa kuwa na tuzo 23.

winners-

Drake ameweka rekodi ya kuwa msanii pekee aliyeshinda tuzo nyingi zaidi za Billboard kwa muda wote, huku Cardi B akiondoka na tuzo 6 na Maroon ameondoka na tuzo 4.

Tuzo za muziki za Billboard (Billboard Music Awards) zimefanyika usiku wa Jumatano ya May 1, 2019 kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden jijini Las Vegas Marekani.

LEAVE A REPLY