Dotnata afiwa na mama yake mzazi

0
235

Muigizaji mkongwe wa filamu, Dotnata amefiwa na mama yake mzazi, Ildegalda Alphonce aliyefariki dunia siku ya Jumatatu katika Hospitali ya Boch, Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Dotnata amesema kuwa kifo cha mama yake kimeacha pengo kubwa katika familia kwani kama mzazi, alikuwa na umuhimu mkubwa kwao, lakini ndiyo mapenzi ya Mungu hawawezi kuyapinga.

Amesema kuwa “Kufiwa na mama siyo jambo dogo, ni kubwa mno, mama yetu ametuachia pengo kubwa na tutamkumbuka sana kwa mengi, ameugua kansa (hakupenda kutaja ya nini) kwa muda mrefu na ameteseka sana kwa kweli ndipo Mungu akaamua kumpumzisha.

Pia amesema kuwa tunaumia sana, lakini inabidi tukubaliane na kilichotokea maana kila nafsi lazima itaonja mauti. Tulimpenda mama yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,”.

Mwili wa mama wa Dotnata ulitarajiwa kusafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera na msiba upo nyumbani kwa dada yake Dotnata maeneo ya Segerea, Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY