Dongo Janja amuweka wazi mpenzi wake

0
252

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ameamua kuweka wazi kuhusiana na mahusiano yake mapya na mwanadada ambaye ni mfanyabiashara Jijini Arusha aitwaye Linna.

Kupitia kurasa wake wa Instagram Janjaro amefunguka kuwa hakuna neno linaloweza kutosha kuelezea hisia zake kwa mwanadada huyo, ambaye alikuwa akimtumia salamu za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Ameanza kwa kuandika “Hakuna neno linaloweza kutosha katika kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu mengine nitakuelezea chumbani.

Pia kupitia akaunti yake ya ameongeza kuandika ‘Kula ushibe, Kisha kaza chaga nakupenda sana”.

Dogo Janja alionekana na mwanadada huyo siku za hivi karibuni lakini kila alipohojiwa hakutaka kuweka wazi juu ya uhusiano wao.

LEAVE A REPLY