Don Cheadle apiga dili kuigiza kama Mugabe

0
67

Muigizaji filamu kutoka Marekani Donald Frank Cheadle Jr aliyeigiza kama Paul Rusesabagina kwenye filamu maarufu ya Hotel Rwanda amepiga chini dili kuigiza kama aliyekuwa Rais Zimbabwe, Robert Mugabe.

Donald Frank Cheadle Jr alipewa ofa ya kuigiza kama Rais huyo kwenye filamu ya “Mugabe” iliyotakiwa kutoka mwaka 2019.

Muigizaji huyo amesema kuwa alipigiwa simu kuigiza kama Mugabe lakini walitaka aigize kama Muafrika na Mmarekani kwa akaamua akatae ofa hivyo.

Muongozaji wa Filamu hii anatajwa kuwa Director Njagu, aliyetayarisha filamu ya Lobola amesema kuwa anampenda sana muigizaji huyo lakini ameamua kumuacha kutokana na kuwa na waigizaji bora wa kiafrika na siyo kutegemea waigizaji wa Hollywood.

Amesema kuwa  “Nampenda Donald ila tumechoka kuwa na wageni wanaoigiza kana watu wetu, tuna waigizaji bora hapa nyumbani, pesa zinaenda Hollywood nasio hapa,tumechoka wao kuja kutumia lafudhi feki za Africa,  nimeanza kuifanyia kazi hii filamu, ntatoa taarifa soon”.

LEAVE A REPLY