Domo Kaya amtuhumu Alikiba kuiba kionjo chao ‘Yebaba’

0
136

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amejikuta katika kitimoto baada ya msanii mkongwe wa Bongo Fleva Domo Kaya kumtuhumu msanii huyo kwa wizi.

Tuhuma hizo zimekuja Baada ya Ali Kiba kutoa wimbo wake unaofanya vizuri hivi sasa ‘Kadogo’ ambapo ndani ya wimbo huo anasikika akitumia kidokezo cha ‘Yebaba’ ambacho Domokaya amedai amebuni yeye.

Domo Kaya amemuibukia Ali Kiba na kuwataka wasanii wengine wote hasa wapya kwenye tasnia ya Bongo fleva kuwa wabunifu kwenye kazi zao na sio kutegemea ubunifu wa wengine.

Domo Kaya amesema kuwa haikuwa vibaya kwa Ali Kiba kutumia neno hilo lakini kiukweli alitakiwa kumuomba ruhusa kabla ya kutumia kionjo hiko.

Mwanamuziki huyo mkongwe amedai kuwa kama Alikiba angewaomba ruhusa kutumia kionjo hicho basi wamemuachia lakini amefanya vibaya kutumia bila ruhusa zao.

Kwa upande wake Alikiba bado hajazungumzia suala hilo la tuhuma zidi yake kuhusu kuiba kionjo cha wanamuziki hao Domo Kaya na Mandojo.

LEAVE A REPLY