Dogo Janja aweka wazi ujauzito wa Irene Uwoya

0
565

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa mke wake Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ni mjamzito hivi sasa na wakati wowote anaweza akajifungua mtoto wao wa kwanza.

Dogo Janja hivi sasa anatamba na wimbo wake mpya uonaoitwa ‘Wayu wayu’ uliojizoelea umaarufu baada ya yeye mwenyewe kuwa video queen humo ndani akiwa amevaa kama mwanamke na kupaka make up kitendo kilicho amsha hisia za watu wengi.

Dogo Janja amesema kuwa kwasasa anatarajia mtoto kutoka kwa mke wake Irene Uwoya baada ya kushika ujauzito.

Pia Dogo Janja aliweka wazi kuwa endapo atazaa mtoto wa kiume basi atapendelea kumuita Aboubakary jina la marehemu baba yake lakini endapo atakuwa wa kike basi atamuachia mama yake ampe jina.

LEAVE A REPLY