Dogo Janja awatoa thamani wasanii wenzake kisa Nandy

0
292

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema kuwa wasanii wenzake wa Bongo Fleva wamekosa umoja na mshikamano hasa pale mmoja wao anapopatwa na tatizo.

Kauli hiyo ya Dogo Janja imekuja baada ya baadhi ya wasanii kushindwa kumsapoti mwanamuziki mwenzao Nandy aliyekumbwa na skendo ya video yake ya utupu kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Dogo Janja amesema kuwa kwasasa hana Imani na wasanii wenzake ambao wameonekana kufurahia kitendo hiko huku wakiombea msanii huyo afungiwe.

Kupitia akaunti yake Instagram ameandika.

 “Nahisi ninaweza kumaindiwa leo na wasanii wenzangu ila lazima mtu aanze ndo hili donda ndugu litapona. Wasanii sisi ni masinichi sana aisee, baada ya hii ishu ya Nandy ndo nimepata uhakika. Wakati wa ishu ya Roma nilianza kuliona jinsi kwenye makundi pembeni watu kibao walikuwa wanafurahi tena maneno kibao kama atakoma, amezoea huyo. Jana na juzi nimekaa na watu wasanii wakubwa tu na wote walikuwa wanasema bora limemtokea Nandy hili angalau spidi za show zitapungua, bora BASATA ingemfungia miezi 6 apotee kidogo, walikuwa wanapiga story kama utani ila moyoni nimefikiria sana,“

Pia amemalizia kuandika “Wasanii tuache roho mbaya, wote sisi maskini tunahangaikia ugali. Tukipata ajali kazini, tusiombeane mabaya tutafute amani, vita iwe kwenye kazi jamani,“.

LEAVE A REPLY