Dogo Janja amwagia sifa Young D

0
32

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amempongeza na kumsifia mwanamuziki mwanzake Young D baada ya kuachia EP yake hivi karibuni.

Dogo Janja ameshea ‘EP’ ya Young Dee huku akimnyooshea mikono juu kwa kumwita mfalme wa wasanii wote wa kizazi hiki cha vijana kwenye muziki wa Bongo Fleva.

“Kati ya watu niliokutana nao ambao ni Walimu, huyu chalii Youngdaresalama yumo! bonge la EP kamanda, Mfalme wa Young Generation” ameandika Dogo Janja

Baada ya Post hiyo rapa Young Dee akajibu kwa kuandika kuwa “Young King thanks mwanangu”.

Kwa kauli hizo inaashiria kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya wasanii yao na wamemaliza utata wa muda mrefu uliosemeakana kwamba wasanii hao hawana stori wala maelewano mazuri.

LEAVE A REPLY