Dogo Janja amvalisha pete ya uchumba mpenzi wake

0
61

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa sasa ambaye ni mfanyabiashara kutoka mkoani Arusha aitwaye Linnahonnah.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kupostiwa kwa kipande cha video fupi katika ukurasa wa mtandao wa Instagram wa msanii Linah Sanga, ambayo inaonyesha Dogo Janja akipiga goti kwenye boti na kumvalisha pete mchumba wake huyo.

Linah Sanga ameandika kwa kumpongeza Dogo Janja baada ya kufanikisha kufanya tendo hilo kwa mpenzi wake.

Madee, Linah na Recho ni baadhi ya wasanii ambao wameenda visiwani Zanzibar kula bata pamoja na kusheherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mpenzi huyo wa Dogo Janja.

Kabla ya kuwa kwenye mahusiano na Quenlinnatotoo Dogo Janja alikuwa kwenye ndoa na msanii wa filamu Irene Uwoya, pia amekuwa msanii wa kwanza kumvalisha pete mpenzi wake.

LEAVE A REPLY