Dogo Janja akanusha kununuliwa gari

0
24

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amekanusha taarifa za kununuliwa gari na msanii mwenzake Madee ambapo amesema kuwa taarifa hizo ni za kuzusha.

Dogo Janja amekanusha taarifa hiyo baada ya kusambaa kwa habari kwenye mitandao ya kijamii kuwa amenunuliwa gari na Madee.

Janja amesema kuwa hajawahi kununuliwa gari lolote, hivyo watu waache kuzusha mambo wasiyoyajua kwa kuwa gari zote huwa ananunua kwa pesa yake.

“Madee ni kweli anafanya biashara ya magari hilo nakubali, lakini sijawahi kununuliwa gari na Madee, huwa akileta gari kama nimelipenda, natoa pesa yangu mfukoni nanunua.

Janja amesema kuwa Watu waache kuzusha mambo wasiyoyajua, mtu afanye uchunguzi kwanza ndipo waandike habari za kweli,”.

LEAVE A REPLY