Dogo Janja afungukia biashara zake

0
149

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa mbali na kufanya muziki lakini pia ni mfanyabiashara.

Mwanamuziki  huyo amesema hayo baada ya kuulizwa kama anajihusisha na kazi nyingine mbali na muziki wake anaofanya kwasasa.

Dogo Janja ambaye anafanya vyema kwenye tasnia ya muziki nchini ameweka wazi kuwa pamoja na kuupenda muziki Lakini anaamini ni vyema Kuwa na kitu kingine cha kufanya.

Dogo Janja amesema kuwa amekuwa akifanya biashara zake nje ya muziki wake ambazo zimekuwa zikimwingizia kipato kizuri na kujivunia kuifanya kwa moyo mmoja.

Amesema kuwa anafurahi anafanya biashara ambazo zinamlipa nje ya muziki wke, hivyo anafurahia kile anachokifanya kwa kuwa biashara zake zimekuwa na manufaa makubwa kwenye maisha yake.

LEAVE A REPLY