Dogo Janja afunguka suala ya kupata mtoto

0
26

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa mipango ya kupata Mtoto ipo ila anajipanga kwanza na hataki kukurupuka kisa maneno ya Watu.

Dogo Janja ambaye yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na msichana wa Arusha ambaye ni mfanyabiashara mkubwa mkoani humo.

Dogo Janja amesema kuwa Maisha ni kufurahia Maisha, leo kesho hatupo ntaenda kumwambia nini Mungu, tabasamu zinavicha mambo mengi sana, kuhusu kussuport biashara zake mambo yake ni binafsi sana na nina heshimu sana privacy za Mke wangu”.

Kuhusu Mtoto, Dogo Janja amesema kuwa huwezi kuzaa kwa ajili ya Watu, sina target ya kuwa na Watoto zaidi ya watatu nadhani wawili wananitosha, lazima nijipange” – Janjaro.

Dogo Janja kwasasa yupo kwenye mahusiano ya msichana huyo baada ya kuchana na muigizaji maarufu wa Bongo Movie, Irene Uwoya.

LEAVE A REPLY