Dogo Janja afunguka maisha yake ya utotoni

0
52

Mwanamuziki wa Hip Hop, Dogo Janja amesema kuwa alijaribu kuvuta bangi ila kilichomtokea ni kuchekacheka kila wakati hivyo akaona haimkubali na kuamua kuacha.

Dogo Janja amesema kuwa toka wakati huo hajawahi kutumia tena bangi kwa kuwa akikua kilevi kizuri kwake kwani kilimletea shida sana wakati huyo.

Amesema kuwa “Mimi sivuti bangi, ningetaka kuvuta ningefanya tangu zamani kwa sababu nilikulia mazingira ya hivyo na niliona madhara yake, nilijaribu mara moja nikawa nacheka tu nikaona hainikubali”.

Dogo Janja ameongeza kuwa “Nisingekuwa mwanamuziki basi ningekuwa Mwakinyo fulani hivi au ningekuwa muhuni ambaye ningekuwa nimeshafukiwa, lakini sasa hivi nikiwa Arusha huwa nawatuliza vijana wenzangu wanaopanga uhuni.

LEAVE A REPLY