Dodo ya Alikiba yaweka rekodi Youtube

0
164

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameweka rekodi ya ngoma yake ya Dodo kukaa Youtube Trending kwa muda mrefu kuzidi ngoma yoyote iliyotoka mwaka huu.

 

Alikiba alifikisha siku ya tisa kukaa Youtube Trending kwa Tanzania tangu kutoka kwa ngoma hiyo Aprili 8, mwaka huu na kuendelea kufanya vizuri.

 

Ngoma kama Gere ya Tanasha na Diamond, Jeje ya Diamond nazo zilikaa kwa zaidi ya siku nne kwenye trending, lakini hazikuwa muda mrefu kuishinda Dodo ya Alikiba.

 

Hii ni rekodi kubwa zaidi kwa Alikiba kwa miaka ya hivi karibuni, kwani kazi zake nyingi alizotoa hazikuwahi kukaa kwenye trending kwa muda mrefu kama ilivyo kwa Dodo.

 

Kuhusu rekodi hiyo Alikiba alisema kuwa mashairi ya wimbo huo ni mazuri, biti na melodi ni vitu ambavyo vinaibeba sana wimbo huo.

LEAVE A REPLY