Dkt. Slaa amshukuru Rais Magufuli kumteua kuwa Balozi

0
213

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Balozi wa Tanzania.

Dkt. Slaa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, na ambaye aliwahi kugombea nafasi ya Urais kupitia chama hicho alijiuzulu nafasi yake hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuondoka nchini.

Muda mfupi baadaye Dkt. Slaa alitangaza kutojihusisha tena na siasa za hapa nchini na akawa anaishi nchini Canada pamoja na mpenzi wake Josephine Mushumbusi.

Dk. Slaa, ambaye kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2015 aliweka wazi kuwa anafanya kazi zaidi ya mbili ili aweze kujipatia kipato kitakachomuwezesha kumudu gharama za maisha nchini humo.

Alitaja kuwa kwa sasa anafanya kazi ya Mshauri wa Mauzo (sales Advisor) pamoja na kutoa ushauri (consultancy).

Kufuatia uteuzi huo wa Dkt. Slaa kuwa Balozi uliofanywa na Rais Magufuli, taaarifa kutoka ikulu imeeleza kuwa zoezi la kuapishwa kwake litafuata baada ya kukamilishwa kwa taratibu.

LEAVE A REPLY