Dkt Massaburi kuzikwa Jumatatu Chanika

0
172

Dk Didas Masaburi (52) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika chuo chake Chanika, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Dk Masaburi ambaye alikuwa mwanasiasa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na homa ya ini.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Ojambi Masaburi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Chanika, Dk Masaburi aliwahi kupelekwa nje ya nchi mara mbili kwa ajili ya matibabu.

Alisema Dk Masaburi alipelekwa Muhimbili Jumapili na hadi mauti yanamkuta alikuwa amelazwa hospitalini hapo.

Atazikwa chuoni kwake “Institute of Procurement and Supply” kama alivyoacha wosia kuwa atakapofariki azikwe eneo hilo.

Mwaka 2010, Dk Masaburi alichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni na Desemba 23, akachaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam katika uchaguzi ukliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini hapo.

Mwaka 2015, Dk Masaburi aligombea ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM ambako alishindwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Saed Kubenea.

LEAVE A REPLY