Dkt. Kigwangalla azitaka sekta za afya kutoajili watu wasiokuwa na vyeti kutoka mabaraza ya maabara

0
167

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka waajiri wote katika sekta ya umma na sekta binafsi kutowaajiri watalaamu ambao hawajasajiliwa.

Pia amewataka kutowaajiri watumishi ambao hawana vyeti vya usajili kutoka katika mabaraza ya kitaaluma husika.

 Naibu Waziri Kigwangala ameyasema hayo  jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa baraza la wataalam wa huduma za maabara za afya ambapo amesema baraza hilo linakamilisha utaratibu wa kuwapa leseni wataalam wasio na taaluma ya maabara za afya, walioruhusiwa kisheria kufanya baadhi ya vipimo vya maabara ikiwemo vipimo vya haraka vya maambukizi ya ukimwi na malaria.

 Dkt Kigwangalla amesema kuzinduliwa kwa baraza hilo kutasaidia katika kuboresha huduma za afya katika jamii ili kukidhi viwango vinavyotarajiwa na hivyo kuboresha afya na maisha ya wananchi wote pamoja na kutoa fursa ya kujiendeleza, hivyo kuongeza weledi katika kutoa huduma za afya.

 Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya, ni chombo cha kisheria kilichowekwa na serikali ili kuwatambua na kuwasajili Wataalam wa Maabara za Afya ya Binadamu, kusimamia ubora wa utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya binadamu, kuchukua hatua za kisheria kwa wakiukaji wa sheria, na kushauri serikali katika kuboresha huduma za maabara kwa wagonjwa.

LEAVE A REPLY