Dimpoz asimulia alivyonusa kifo

0
61

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa madaktari wa Ujerumani walimwambia alibakiza wiki moja tu angefariki dunia kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

Ommy Dimpoz alifanyiwa upasuaji wa koo nchini Afrika Kusini ambapo alikundulika kuwa amekunywa sumu na kumletea matatizo ndani ya mfumo wake wa chakula na kushindwa kula vizuri.

“Vipimo vya Daktari ilionekana kuna sumu nimekula au nimekunywa na ndiyo iliyoleta tatizo hilo na majibu hayo nilipata katika hospital zote nilizopita Mombasa, South Africa pamoja Ujerumani.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa anamshukuru Mungu kwasasa anaendelea vizuri maana mwaka jana hakuwa mzuri kwa upande wake hivyo anabudi kumshukuru mungu kwani sasa anaendelea vizuri.

Ommy amesema kuwa kabla hajafanyiwa upasuaji wa kwanza, madaktari walimuambia upasuaji utakuwa mkubwa, hivyo wakampa muda wa kukaa na kujitafakari tena na kuongea na familia yake kuhusu suala hilo la upasuaji.

Pia amesema kuwa upasuaji wake ulichukua saa sita mpaka kumi na moja na madaktari walikata tumboni mpaka karibia na kifua, pia shingoni na sehemu zingine na walifanya hivyo ili kupandisha tumbo juu na vitu vingine ili kuhakikisha wananusuru maisha yake.

Vile vile ameongeza kwa kusema kuwa wakati alivyokwenda Ujerumani walivyomcheki wakagundua usaha umezidi na unakaribia kuingia kwenye maini na alibakiza wiki moja tu kama angechelewa angeweza kufariki dunia.

LEAVE A REPLY