Dimpoz arejea nchini baada ya matibabu

0
97

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amerejea nchini akitokea kwenye matibabu yake baada ya kuugua kwa muda mrefu alipokuwa amelezwa nje ya nchi.

Ommy Dimpoz amesema kuwa haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.

Mwanamuziki huyo ameongea hayo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam wakati akirejea nchini.

Dimpoz amesema kuwa anamshukuru mungu hali yake kwasasa inaendelea vizuri tofauti na hapo awali hivyo ana budi kutoa shukrani zake kwa mungu na mashabiki wake waliomuombea.

Mwanamuziki huyo alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya koo mpaka kupelekea kufanyiwa upasuaji mkubwa nchini Afrika Kusini pamoja na matibabu mengine yaliyofanyika nchini Ujerumani.

LEAVE A REPLY