Didi Akinyelure ndiye mshindi wa tuzo ya Komla Dumor 2016

0
135

Mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha CNBC cha Nigeria kinachorusha matangazo yake barani Afrika, Didi Akinyelure amechaguliwa kuwa mshindi wa tuzo maalum inayotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC kwaajili ya kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa shirika hilo Komla Dumor.

Didi ambaye ni mtangazaji wa habari za biashara kwenye kituo hicho anatarajia kujiunga na idhaa ya BBC ya London kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.

Mmoja wa majaji ambao walimpigia kura Didi katika ushindi huo, Josephine Hazeley amemsifu Didi kwa utangazaji mzuri wa habari za biashara ambazo pia marehemu Dumor alipenda kuzitangaza.

Baada ya kutangazwa kuwa mshindi Didi alisema ‘Dumor ni mmoja ya watu waliokuwa wakinivutia sana kwenye kazi zao. Alikuwa akielezea habariza Afrika kwa mapenzi na mguso mkubwa kwa bara hili huku akizipa uzito unaowiana pande zote na alikuwa akiwavutia wengi’.

Tuzo ya Komla Dumor ilianzishwa ili kuuenzi mchango wa mtangazaji huyo kwa shirika la BBC na tuzo ya kwanza ilitwaliwa na mtangazaji kutoka Uganda Nancy Kacungira.

Dumor aliyekuwa mtangazaji wa BBC World News alifariki ghafla mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 41.

Tuzo: Hayati Komla Dumor enzi za uhai wake
Tuzo: Hayati Komla Dumor enzi za uhai wake

 

LEAVE A REPLY