Diamond Platnumz ‘Simba’ na Rayvanny ‘wamfikisha’ SALOME AFCON

1
3659

Simba wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz akiwa na nyota wa WCB, Raimond a.k.a Rayvanny jana walifunika kwa performance yao ya ngoma SALOME wakati wa utoaji wa tuzo za Mchezaji Bora wa Afrika 2016.

Unajua zawadi ya SALOME ilikwenda kwa nani? Ni Mahrez, staa wa Leicester City ya Uingereza.

Hebu mcheki Simba na Rayvanny wakimkabidhisha SALOME kwa watazamaji.

Kutokana na kupewa nafasi ya ku-perform LIVE mbele ya waheshimiwa wengi, Rayvanny alionyesha shukrani yake kwa Diamond Platnumz na WCB Crew kwa pamoja na akaandika:

‘Kweli Mungu Akipanga yanatimia. @diamondplatnumz Upendo wako,kujali nakupoteza muda wako kwa ajili ya vijana wako hio ndio siri pekee ya safari yako kuwa ndefu zaidi na Mungu akuongezee zaidi na zaidi uzidi kwenda mbaaaali’.

‘HUA SIAMINI NIKIKUMBUKA NILIKOTOKA NAONA NI NDOTO!!! Sijutii kua Na Uongozi Imara Sana (WCB) @babutale @sallam_sk @mkubwafellatmk @kameboy_j @ricardomomo THANKS ALOT ABUJA NIGERIA AND THE WHOLE #GLOCAFAWARDS CREW’

1 COMMENT

LEAVE A REPLY