Diamond Platnumz na Parimatch walivyowasaidia yatima

0
30

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch kwa kushirikiana na balozi wao Msanii Diamond Platinumz wametoa msaada katika vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Dar er salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana amesema Kampuni ya Parimatch inapenda umma utambue kuwa imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii hususani katika nyanja za elimu, michezo, na mazingira.

Parimatch Imeanza na idara ya elimu kwa watoto wenye mahitaji muhimu kwa kuangazia baadhi ya mahitaji yao.

Katika mahitaji yao tutawapa chakula na nyenzo za kujifunza ili kuweza kuendana na kasi ya teknolojia na kujiandaa vyema na mahitaji ya soko la ajira au kujiajiri kwa kuwapa runinga, jenereta pamoja na Mifumo kamilifu itakayounda maabara za Kompyuta ili kusudi viweze kuwaendeleza katika masuala ya elimu na kujifunza’, amesema.

Balozi wa Parimatch Tanzania Diamond Platnumz ameweka wazi furaha yake ya kufanya kazi na kampuni hiyo yenye misingi ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hususani yatima na misingi ya kusaidia jamii katika nchi zote zaidi ya 15.

Diamond amesema, Tutaanza na vituo viwili kuwapa mahitaji ya chakula ambayo bila hivyo huwezi kusoma, lakini mada kuu elimu.

LEAVE A REPLY