Diamond Platnumz na Ali Kiba nani aliuanza ubaya?

2
1552

Historia ya muziki wa mastaa Ali Kiba a.k.a King Kiba na Diamond Platnumz inaonyesha kuwa wawili hawa ni wasanii marafiki ambao wapenzi wa muziki walitarajia mambo makubwa ya pamoja kutoka kwao, lakini sasa hali ni tofauti ‘HAWAIVI CHUNGU KIMOJA!.’

Ugomvi wao ‘kisanii’ umetokana na nini?

Diamond aliwahi kukaririwa akidai kuwa:

‘Nilitaka kuingiza sauti kwenye wimbo wa Kiba, Single boy wakati huo tulikuwa studio lakini lakini alikataa na kusema kuwa nataka mteremko.’

Lakini Kiba naye aliwahi kunukuliwa akisema:

Niliingiza sauti kwenye limbo wa Diamond, ‘Lala Salama’ lakini nilistuka sana limbo ulipotoka kuona sauti yangu imefutwa’

Nani mbaya kati ya hawa? HAIJULIKANI na kila mmoja ana ukweli wake.

Kila mmoja ana ‘team’ yake na team hizi zimekuwa zikiwanyima ushindi mastaa hawa licha ya ukweli kuwa zinatafsiriwa kama kipimo cha mafanikio yao pamoja na kuonekana kama nguvu (mtaji) wa mafaniko hayo.

Lakini kwa nyakati tofauti mastaa hawa wameombeana kura baina yao kwenye tuzo mbalimbali.

Nani aliuanza ubaya? Hawawezi kusameheana?

 

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY