Diamond Platnumz kusaidia kaya masikini

0
38

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameahidi tena kufanya mambo makubwa kwa wananchi wenye kipato cha chini kwa kusaidia kuboresha makazi na nyumba zaidi 100 za familia tofauti tofauti.

Diamond kwa kushirikiana na uongozi wa kampuni ya rangi ijulikanayo kama Coral Paints wameahidi kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini ambao hawajaweza kumalizia ujenzi wa nyumba zao.

Mpango huo unalenga kuwasaidia wananchi hao kupaka rangi nyumba zao ziwe katika muonekano mzuri.

Amesema kuwa “Unajua nyumba zetu za uswahilini na kule kwa wenzetu washua hazina tofauti ila wanapotupiga bao ni katika umaliziaji uchaguzi wa rangi wanaoufanya na mbwembwe tu na tumegundua kuwa hizi nyumba za uswahilini tunazoziona nyingi ni nzuri ila zimekosa rangi na umaliziaji mzuri tu.

“Kuanzia siku hii ya leo sisi kama Coral Paints kulidhihirisha hilo kwa ndugu zetu, watanzania wenzetu, mikoa na mitaa mbalimbali tutafi kia nyumba zaidi ya 100.

LEAVE A REPLY