Diamond Platnumz kujenga shule ya mpira

0
233

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa yupo katika mazungumzo na mchezaji maarufu wa mpira kutoka Cameroon, Samuel Eto’o kutaka kujenga shule ya mpira nchini Tanzania.

Mwanamuziki huyo alituimbuiza katika sherehe za tuzo za shirikisho la mpira barani Afrika, (CAF) iliyowaburudisha watu wengi wakiwemo meneja Gianni Infatino na wachezaji wengine.

Katika kurasa yake ya tweeter, Diamond amebainisha kuwa na mazungumzo na Eto’oo kwa muda mrefu sasa ya kutaka kuanzisha klabu ya mchezo wa mpira kwa sababu ukanda wa Afrika mashariki una wachezaji mpira wa baadae wenye uwezo.

Diamond amesema ”Hapo awali, nilidhani kuwa kujihusisha na maswala ya michezo ni kitu kisichokuwa na faida, lakini sasa naona ni jambo la faida sana…Huko mbeleni? Nitakuwa mmiliki wa timu yangu mwenyewe, ambayo tayari inafanya biashara kwenye premiere ligi kwa sababu sitaki kuanza mwanzo kabisa.”

Mwanamuziki huyo hakutoa muda kamili wa mradi huu lakini ni wazi kabisa kuwa anataka kununua moja ya klabu zilizopo sasa au mchezaji maarufu.

Katika mitandao ya kijamii watu wengi wameonesha kufurahishwa sana na jambo hili na kumtakia kila la heri kwenye mradi huo.

 

LEAVE A REPLY