Diamond Platnumz ‘kuitosa WCB’ akipata ofa aitakayo?

1
1119

Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amweka hadharani kuwa ‘alikataa kusaini kwenye lebo ya staa mkubwa wa muziki nchini Marekani, Jay Z’.

Diamond ameyaeleza hayo katika kile kinachoonekana kama kujionyesha kuwa yeye ni msanii staa zaidi kwa Tanzania.

‘Wakati nilipokuwa chini ya BET, lebo kubwa ya Marekani inayomilikiwa na Jay Z ilinifuata ikiwa na ofa nzuri na kutaka kunisainisha lakini nilikataa’. Amesema Diamond.

‘Ukiacha lebo hiyo, kuna lebo nyingine kubwa za Marekani na Ulaya ambazo zilitaka nifanye kazi chini yao lakini nilikataa pia na siku zote nimekuwa nikilenga kukuza muziki wangu na sio kusainishwa na lebo halafu kila kitu wamiliki wao’. Ameongeza Diamond

‘Kwa muziki wa Marekani kupata collabo ni kitu cha kawaida sana, unachopaswa kuzingatia ni kuwa muziki ni biashara hivyo utakayemtaka mfanye collabo atahitaji kujua yeye atanufaika vipi na kazi hiyo, hawana shida ya umaarufu’.

‘Kama mtu akitaka kunisaini lazima akubali kuwa muziki wangu nataka uuzike kama unavyouzika muziki wa mastaa wakubwa kama Jay Z na Kanye West, akija na mkakati huo, ntakubali kusaini’.

1 COMMENT

  1. Comment:KWELI WE DIAMOND NIMEKUKUBALI HAUNA TAMAA YA VICENT VYAO,NA WALA HAUTAKI KUUPOTEZA MUSIC WAKO,HONGERA SANA JEMBE KOMAA ,TUNAKUKUBALI SANA!!!

LEAVE A REPLY