Diamond Platnumz kufunika na ‘DIAMONDS ARE FOREVER Season II’

0
851

Unaikumbuka shoo ya ‘DIAMONDS ARE FOREVER’?

Umei-miss?

Baada ya kupotea kwa miaka kadhaa, lebo ya WCB chini ya mameneja wake wanairudisha tena shoo ya DIAMONDS ARE FOREVER.

Mmoja wa mameneja wa lebo hiyo, Sallam ametangaza kurudi tean kwa shoo hiyo na kutangaza kuwa mwaka huu itafanyikia uwanja wa taifa ili kuruhusu watu wengi zaidi kumuona staa wao Diamond Platnumz.

Kwa mara ya kwanza, Diamonds Are Forever Concert lilifanyika mwaka 2012 kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Team ya WCB imekuwa timu inayoongoza kwa ubunifu wa harakati za burudani na promosheni kwa lebo hiyo inayoongozwa na kinara wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz.

Hata hivyo Sallam hakutoa taarifa kiundani kuhusu tarehe ya kufanyika kwa onyesho hilo na endapo kuna washiriki wan je ya lebo ya WCB ambao watashirikishwa.

Diamond Platnumz pia mbali ya kuwa na tamasha la Diamonds are Forever pia hushirikiana na mpenzi wake Zarina Hassan a.k.a Ze Boss Lady kwenye tamasha jengine la ALL WHITE PARTY!

diamond

LEAVE A REPLY