Diamond Platnumz aweka wazi mdhamini wa Wasafi Festival

0
185

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amewaka wazi kuwa kampuni ya Pepsi ndio itakuwa mdhamini wa Tamasha la Wasafi Festival ambalo linatarajia kuanza Novemba 24 mwaka huu mkoani Mtwara.

Diamond Platnumz amethibitisha hayo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kuwa kinywaji hicho ndicho kitakuwa mdhamini wa Tamasha hilo kubwa la kimuziki nchini.

Naomba Nianze kuwaleta Kwenu Wadhamini wa #WasafiFestival2018 sasa!!!!….Kwanza kabisa naomba Tuwakaribishe Rasmi @Pepsi_tz katika #WasafiFestival2018… Asante sana @Pepsi_tz kwa kuthamini Sanaa yetu… Asante kwa Kuamini katika Vijana… asante kwa Kuamini #WasafiFestiVal208 ….Uwepo wako ndani ya #WasafiFestival2018 Unathamani kubwa sana, na Utaenda Fungua Milango ya Vijana wengi Wenye ndoto ya kufanikiwa kupitia sanaa….. Nasemaje Wadau kuanzia sasa hii ndio soda yetu Rasmi ya #WasafiFestival2018 , na Ukiwa kama Mpenda burudani ya haki naomba kwa Kuwapa shukran kwa Kuisapoti #WasafiFestival2018 kuanzia sasa sie woteTufyekelee mbali visodasoda Vingine….. yani Soda yetu iwe ni Pepsi tu!!!.. na ndugu zake kina Mirinda Nyeusi, 7Up!!!!…😋😋😋😋 Kama Mirinda Nyeusi nishainywaga sana kwa Kujificha ila Round Hii Tutakutana na Pakiti za @DiamondKaranga

#Pepsitz #LiveForNowTZ #LiveForNow
@Pepsi_tz @Pepsi_tz
PEPSI USIIICHEZEE WEWE!!!!!!

LEAVE A REPLY