Diamond Platnumz awakimbiza Youtube

0
32

Wanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Harmonize na Rayvanny ndio wasanii pekee wa Tanzania wanaounda 15 bora wanaotazamwa zaidi kimataifa kwenye Youtube.

Orodha ya wasanii hao inaongozwa na Burna Boy akiwa ametazamwa na watu Milioni 435.57 namba mbili ni Diamond Platnumz watu zaidi ya Milioni 291.98.

Kwenye orodha hiyo namba 9 ikishikwa na Harmonize akiwa na watu zaidi ya Milioni 138.98 Rayvanny akiwa namba 10  akitazamwa na watu zaidi ya Milioni 133.69.

Pia Diamond Platnumz ameingia kwenye 15 bora ya wasanii wanaotazamwa zaidi Kimataifa kwa Bara la Afrika kwa ujumla akiwa namba 14.

Kwenye Orodha hiyo Hamo Bika kutoka Misri anaongoza akiwa na watazamaji zaidi ya Bilioni 1.14 kwenye mtandao huo wa Youtube kwa kutazamwa na watu wengi.

LEAVE A REPLY