Diamond Platnumz athibitisha ujio wa kolabo na G Nako

0
47

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amethibitisha kuwa kwenye kolabo ya pamoja na mwanamuziki wa Bongo Fleva, G Nako kutoka kundi la Weusi.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii Diamondo Platnumz katika uwanja wa maoni wa post yake alifichua uwepo wa kolabo yake na G Nako.

Uthibitishilo wa kuwepo kwa kolabo hii umekuwa ghafla isibainike moja kwa moja ni yupi aliyemshirikisha mwenzake kati ya wakali hao huku mashabiki wakionesha hamu ya kuutamani ujio huo hivi karibuni.

Kama wimbo huo utatoka ndiyo itakuwa ngoma ya kwanza kufanyika kwa kolabo ya wawili hao katika muziki wa Bongo Fleva kwa siku za hivi karibuni.

Diamond Platnumz juzi kati alikuwa nchini Malawi kwenye tamasha la Sand lililowakutanisha wasanii mbali mbali kwenye tamasha hilo nchini humo.

LEAVE A REPLY