Diamond Platnumz athibitisha ujauzito wa Tanasha

0
711

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amethibitisha kuwa mpenzi wake wa sasa ambaye ni raia wa Kenya, Tanasha Donna, ana ujauzito wa miezi saba.

Diamond amethibitisha hilo wakati wa hafla maalum ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama yake mzazi, Bi. Sandra na mpenzi wake, Tanasha Dona iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

Chibu ni baba wa watoto watatu, Tiffah na Nilan, aliozaa na mfanyabiashara Zari ambaye waliachana mwaka jana 2018, ambaye ni raia wa Uganda.

Mtoto mwingine ni Dylan ambaye amezaa na mwanamitindo ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto.

Staa huyo kwa sasa anatarajiwa kupata mtoto wa nne baada ya kumpachika ujauzito mpenzi wake Tanasha ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha Radio nchini Kenya.

Mimba ya Tanasha ilianza kuzungumziwa siku za hivi karibuni baada ya mashabiki wa Diamond kuona hali imebadilika kwa dada huyo ambaye ameshajizolea umaarufu hapa Bongo.

LEAVE A REPLY