Diamond Platnumz amtia moyo Young Killer

0
144

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz awatia moyo wasanii wa Hip Hop baada ya kuikosa 10 bora ya wasanii waliotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Diamond Platnumz ameijibu comment ya Young Killer ambayo aliiacha kupitia kwenye post yake ya List ya wasanii 10 walioongoza kwenye platform ya YouTube kwa mwezi wa 4,2020.

Young Killer akiandika “HipHop tu ndio imekosa hapo!! Daah Oi mwanangu Nikki Mbishi tunafanyaje?”. Diamond alimjibu Young Killee kwa kuandika “Kila kitu mbona kinawezekana Msodoki”

Hii si mara ya kwanza kwa sanii wa Hip Hop kuachwa nyuma zinapotoka takwimu mbalimbali kutoka kwenye platforms za usambazaji wa muziki.

Kwenye orodha hiyo ya wanamuziki wa Bongo Fleva ambao wametazamwa sana kwenye mtandao wa Youtube ambapo hakuna hata mwanamuziki mmoja wa hip hop.

LEAVE A REPLY