Diamond Platnumz amshukuru Alicia Keys

0
116

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemshukuru mwanamuziki wa Marekani, Alicia Keys kwa kumpa fursa ya kushiriki katika albam yake inayotarajiwa kutoka karibuni.

Amempongeza mwanamuziki huyo wa muziki wa R&B na mwanamuziki Swizz Beatz kupitia akaunti yake ya Instagram amewashukuru kwa kumpa nafasi hiyo adimu.

Mashabiki wa Diamond, kupitia mitandao mbalimbali, wanahisi nyota huyo aliyeipa nchi yake na Afrika Mashariki umaarufu katika muziki, alistahili kupeta nafasi hiyo.

Wakati huohuo, habari hiyo imetokea kipindi kifupi baada ya mzazi  mwenzake na staa huyo, Tanasha Donna, mrembo, raia wa Kenya, kumvaa mwanamziki wa kike Mtanzania, Zuchu, na Diamond, akidai “waliiba” maneno ya wimbo wake wa Radio.

LEAVE A REPLY