Diamond Platnumz ampongeza Harmonize kuachia Albam

0
311

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amempongeza mwanamuziki mwenzake, Harmonize baada ya kuzindua Albam yake mpya iitwayo Afro East siku ya Jumamosi.

Harmonize mwaka jana alitangaza kuachana na lebo ya WCB chini ya Diamond Platnumz na tangu mwanamuziki huyo kuondoka hakukuwa na ukaribu wa wawili hao toka kutoka kwake.

Diamond ambaye ndiyo alimtoa kimuziki mwanamuziki huyo kwani Harmonize alikuwa mwanamuziki wa kwanza kusainiwa na lebo ya WCB amempongeza mwanamuziki huyo kutokana na albam hiyo.

Diamond amewaomba watanazania kumsapoti Harmonize kwa kuinunua Albamu yake hiyo kupitia mitandao mbali mbali ya uuzaji wa Albam mitandaoni.

Albam ya Harmonize ‘Afro East’ ina jumla ya nyimbo 18 ameizundua rasmi siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa Albam hiyo ulihudhuriwa na wasanii mbali mbali pamoja na viongozi wa Serikali pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

LEAVE A REPLY