Diamond Platnumz ampongeza Babu Tale

0
94

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amempongeza meneja wake, Babu Tale kwa kuapishwa na kuwa mbunge wa Morogoro Kusini baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu.

Diamond amepongeza hatua ya mwanzo wa safari ya Meneja wake, Babu Tale kuwatumika wakazi wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki baada ya uapisho rasmi wa wabunge, Novemba 10 2020 Bungeni mjini Dodoma.

Diamond alisisitiza kuwa hana shaka kabisa na Babu Tale kwa wanaMorogoro na kuongeza kuwa mafaniko yake na wenzake chini ya uongozi wa meneja huyo ni ishara ya kuwa jimbo la Morogoro limepata mtu sahihi kwa safari ya maendeleo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Toka mwanzo nasema sina Mashaka na wewe Kama uliweza kutuongoza Vijana wengi kwenye sanaa na Shughuli mbalimbali mpaka leo tumefikia hapa. Pia ameendelea kwa kuandika Basi najua Morogoro Kusini Mashariki iko Mikono salama”.

LEAVE A REPLY