Diamond Platnumz ahairisha Tour yake barani Ulaya kisa Corona

0
353

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amehairisha Tour yake ya kimuziki barani Ulaya kutokana na hofu ya ugonjwa wa Corona vinavyoenea barani humo.

Virusi vya Corona vinazidi kusambaa kila kukicha huku sekta mbalimbali zikiathirika kwa kiasi kikubwa sana duniani hivyo kuamua kuathiri mambo mbali mbali yenye mkusanyiko.

Taarifa kutoka kwa meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK ni kwamba wamelazimika kusitisha shows za Diamond balani ulaya kutokana na hofu ya ugonjwa huo.

Diamond alipaswa kupiga show kwenye miji ya Brussels nchini Ubelgiji, Helsnki nchini Finland, Dortmund nchini Ujerumna na Marseille nchini Ufaransa, kutoka na hayo tarehe ya tour hiyo itatangazwa tena hapo baadae.

Mikusanyiko mbalimbali imepigwa marufuku barani ulaya kama kwenye viwanja vya michezo na starehe kutokana na spidi ya maambukizi ya vurusi hivyo vilivyouwa maelfu ya watu mpaka sasa Duaniani.

LEAVE A REPLY