Diamond Platnumz afikisha watazamaji milioni 900 Youtube

0
593

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka rekodi mpya Afrika kwa kuwa msanii wa kwanza kufikisha watazamaji Milioni 900 kwenye mtandao wa Youtube.

Diamond alijiunga rasmi kwenye mtandao huo mnamo Jun 12, mwaka 2011 huku katika akaunti yake hiyo anayoitumia kuweka maudhui mbali mbali.

Katika akaunti yake ya Youtube wimbo ambao umeangaliwa zaidi kuliko wimbo wowote ule ni Yope Remix aliyoshirikishwa na msanii kutoka nchini DR Congo Innoss’B ambao umetazamwa mara milioni 74 ukifuatiwa na wimbo wa Nana aliomshirikisha Mr Flavour kutoka nchini Nigeria na wimbo wa tatu ukiwa ni Inama aliomshirikisha Fally Ipupa kutoka nchini DR Congo.

Mbali na nyimbo hizo kuonekana kufanya vizuri katika akaunti yake hiyo ya Youtube ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni ameachia wimbo wa JEJE ambao ndio umesaidi kusukuma akaunti hiyo na kufikisha watazamaji hao.

Kuna watu wengi wanajiuliza sana kuhusu Diamond kuonekana kufikisha Watazamaji milioni 900 huku wakifananisha na msanii kama Davido ambaye ana wimbo uliotazamwa mara nyingi zaidi kwenye akaunti yake ya Youtube ambao ni Fall ukiwa na watazamaji milioni 161 ukifuatiwa na IF wenye watazamaji milioni 102 huku Wizkid akitamba na wimbo wake aliomshirikisha Drake Come Closer wenye watazamaji milioni 89.

Watazamaji katika akaunti ya mtu inamaanisha watazamaji wa content zote ulizoweka kwenye akaunti yake haimaanishi wimbo mmoja, na hiyo husababishwa na aidha kuwa na video nyingi kwenye akaunti yako au kuwa na ratio nzuri ya watu wanaotazama kwenye akaunti yako istofautiano sana mfano msanii anaweza kuwa na wimbo uliotazamwa mara miloni hata 100 lakini nyimbo zingine zikitazamwa na watazamaji milioni 3, 4 au 5.

Ukija katika suala lililopo kwa sasa ni kwamba Diamond anaongoza kwa kuwa na watazamaji wengi kwenye akaunti yake ya Youtube ikijumuisha nyimbo na content zote alizowahi kupost kwenye hiyo akaunti yake.

Baada ya Diamond kuwa na Watazamaji (views) milioni 903,908,807  akiwa na Subsriber milioni 3.29 anafuatiwa na msanii kutoka nchini Afrika Kusini Die Antwoord akiwa na watazamaji (views) milioni 893,236,573 mbali ya kugawanyika kwa sasa wasanii kutoka Nigeria P Square wakiwa na watazamaji milini 791,497,698 Davido akifuatia akiwa na watazamaji milioni 544143,482.

LEAVE A REPLY