Diamond Platnumz ‘ainyemelea’ Rolls Roys

1
1914

Staa wa Bongo Fleva ambaye hakuna ubishi kuwa ni ‘WA KIMATAIFA’ Diamond Platnumz anataka kupasua vifua vya watu kwa kila anachotaka kukifanya sasa.

Diamond ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, ameandika maneno yanayoashiria kuwa sio tu yeye ni msanii wa Bongo Fleva, BILIONEA lakini pia yeye haogopi kutumia pesa aliyonayo pindi anapotaka kutimiza ndoto zake.

Diamond ambaye amewahi kukaririwa akisema kuwa anatamani kumiliki gari ghali duniani aina ya Rolls Royce huenda akapata nafasi ya kufanya hivyo kwa sasa.

Hilo limekuja baada ya ku-share video fupi akiwa nchini Marekani ambapo anaonekana akilikagua gari hilo huku akirekodi video ya gari hiyo kwa simu yake ya mkononi.

Diamond Platnumz huenda ameshalinunua gari hilo na huenda likawa njiani kuja Bongo.

Gari aina ya Rolls Royce ni moja ya gari ghali zaidi duniani kwenye vyombo vya usafiri wa nchi kavu huku bei yake ikianzia $300,000 (TZS 660m) hadi $500,000 (TZS 1.1bn).

Gari hilo likifanikiwa kutua nchini litawekwa kibao cha jina la PLATNUMZ badala ya vibao vya namba za gari.

Diamond yuko Marekani kwaajili ya kufanya video ya ngoma aliyeifanya na mkali, Ne-Yo.

Kwa sasa Platnumz amejipa jina jipya na ‘The Rolls Royce musician from East Africa’.

‘Nataka nimiliki gari ya ndoto yangu mwaka 2016, na gari ya ndoto yangu ni Rolls Royce’ aliwahi kukaririwa Diamond Platnumz.

Miongoni mwa mastaa wanaoendesha gari za Rolls Royce ni pamoja na David Beckham, Jeniffer Lopez, Kim Kardashian, The Game na Rick Ross.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY