Diamond na Zuchu wanukia kwenye tuzo za Grammy

0
66

Wasanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zuchu na Rayvanny wanukia kwenye tuzo za Grammy 2020. Wasanii hao wanaweza kutajwa kuwakilisha kwenye vipengele mbalimbali.

Diamond Platnumz kupitia video za nyimbo zake  Jeje na Baba Lao anaweza kutajwa kwenye kipengele cha Best Video of the Year.

Zuchu anaweza kutajwa kwenye kipengele cha Best New Artist huku Rayvanny na Skales wanaweza kuingia kwenye kipengele cha Best World Music Album

Hii ni hatua ya mapendekezo ya Grammy, mashabiki hawatokuwa na uwezo wa kupiga kura kwenye hatua hii bali wanachama wa Grammy ndio watahusika kupendekeza wasanii watakao chuana kwenye vipengele rasmi vitakavyotangazwa hivi karibu.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa January 31, 2021 nchini Marekani na kushirikisha wasanii wakubwa mbali mbali duniani ambapo watamenyana kwenye tuzo hizo.

LEAVE A REPLY