Diamond na Tanasha waamua kuficha mapenzi yao

0
185

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na mpenzi wake Natasha toka Kenya wameamua kuweka mapenzi yao kuwa ya siri.

Natasha alifunguka kuhusiana na wawili hao endapo hawataonekana katika mitandao ya kijamii wakiwa pamoja ni kwamba wameamua kuweka mahusiano yao faragha.

Tanasha ameweka post inayosomeka: “D na mimi tumeamua kuweka mahusiano yetu binafsi nje ya mitandao ya kijamii, tunatazama mambo yajayo na furaha yetu, muda ukifika tutaweka mahusiano yetu hadhara tena” katika akaunti yake ya instagram.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Acha niweke mambo sawa, mimi na D tumefikia maamuzi baada ya kuona kwamba ni mapema sana kuweka mahusiano yetu hadhara kwenye mitandao ya kijamii kwa wakati huu. Kwa hiyo tumeamua kuweka mahusiano yetu faragha kwa muda mpaka tuhisi kwamba tunaweza kwenda hadhara kwa mara nyingine.Mungu awabariki nyote“.

Wawili hao wameingia kwenye mahusiano hivi karibuni mpaka Diamond kutangaza kufunga ndoa na mwanamke raia wa Kenya ifiki Februari 14 mwakani.

 

LEAVE A REPLY